Wednesday, 19 September 2018

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mhe. Amos Makalla amehitimisha ziara yake ya kikazi wilayani Tanganyika.

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mhe. Amos Makalla amehitimisha ziara yake ya kikazi wilayani Tanganyika. 
Amefanikiwa kutembelea tarafa zote 3 na alianza kuongea na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda, madiwani na wadau wa maendeleo mbali mbali wa Tanganyika.
Septemba 3, 2018 aliongea na watumishi na madiwani na Septemba 4, 2018 alifanya ziara ya kikazi Mishamo. Septemba 12, 2018 alifanya ziara ya kikazi Ikola na Septemba 14, 2018 Mkuu huyo alienda Mwese. Hute huko alikuwa nasikiliza kero za wananchi na kufanya mkutano wa hadhara.
Mkuu huyo wa mkoa amewapongeza wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda kwa kujitoa katika shughuli za maendeleo na mapokezi yao yalikuwa mazuri sana. Burudani mbali mbali zilioneshwa na kikubwa zaidi ni namna anavyowatetea wananchi na kuwaahidi kushirikiana nao katika kuwaletea maendeleo.

Wananchi wa wilaya ya Mpanda wamepatiwa hati miliki za kimila kwa ajili

Wananchi wa wilaya ya Mpanda wamepatiwa hati miliki za kimila kwa ajili ya makazi na mashamba. 


Hati hizo zimetolewa kwa vijiji vya Mnyagala na Nkungwi. Jumla ya hati miliki za kimila 1,022 zimwtolewa kwa wananchi wa Tanganyika wakati hati 586 ni za Mnyagala na 436 za Nkungwi.
Hati hizo zimekabidhiwa na kaimu afisa tawala wa Tanganyika Bw. Reginarld Muhango kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Tanganyika. Tukio hilo limefanyika Septemba 15, 2018 katika mnada wa Mnyagala na Nkungwi.
Zoezi hili limeanza kwa kuwaelimisha na kuwashirikisha wananchi kuchangia gharama kidogo za mchakato wa hati. Kila mwananchi amechangia shilingi 50,000 kwa kila hati.
Faida za mwannanchi kuwa na hati za shamba au makazi ni pamoja na kuongeza thamani ya kipande cha ardhi, kukopesheka na kuwa na ulinzi wa kudumu wa shamba lako au kiwanja. Pia hati za kimila hazina ukomo wa umiliki tofauti na hati zingine.
Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ina vijiji 55 na tumeanza na vijiji vilivyofanyiwa mpango wa matumizi bora ya ardhi ambapo vijiji 23 vimefanya mpango huu. Baada ya vijiji hivyo, halmashauri itaendelea kuelimisha na kuhamasisha wananchi wengi kumiliki mashamba na viwanja kwa kuvipima na kupatiwa hati.