Wednesday, 15 August 2018


Mfugaji bora wa ng'ombe za nyama katika maonesho ya nane nane 2018 kwa nyanda za juu kusini mwa Tanzania  Bw. Adolf Andrea (aliyevaa kitambulisho) akionesha cheti kwa maafisa mifugo wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda (Tanganyika). Andrea ametunikiwa cheti na shilingi 2 milioni.


Wakulima wa Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika wakijifunza namna ya kupanda mpunga kwa kutumia mashine. Mashine hiyo  iliyokuwa katika viwanja vya maonesho Mbeya 2018, itakuwa mkombozi wa wakazi na wakulima wa mpunga katika vijiji vinavyounda wilaya ya Tanganyika. Kutoka kushoto ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda, mhe. Hamadi Mapengo akiwa na wananchi wa wilaya ya Tanganyika.