Thursday, 26 April 2018

Timu yakutoka mkoa wa Katavi ikikagua miradi ya vijana inayotarajiwa kuzinduliwa na mbio za mwenge wa Uhuru 2018. (Kutoka kulia ni mratibu wa mwenge wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Mhandisi Alkam Sabuni, Mratibu wa mwenge wa mkoa wa Katavi Bw. Boko Maginje, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw. Romuli Rojas John na Mkuu wa Idara ya elimu Msingi mwl. Kenny Shilumba).


Mwananchi wa kijiji cha Sibwesa Bw. Raymond P. Manjori amekabidhi mbuzi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw. Romuli Rojas John kwa ajili ya shughuli ya mwenge 2018. Wananchi wameshiriki vema kuchangia hali na mali.


Dereva wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw. Adam Osward akipimwa malaria katika zahanati ya Kasekese. Siku ya Malaria imeadhimishwa kiwilaya katika kijiji cha Kasekese sambamba na uzinduzi wa chanjo ya kinga ya saratani ya mlango wa shingo la kizazi kwa wasichana wa umri wa miaka 14.
Mwanafunzi wa shule ya Msingi Kasekese akipatiwa chanjo ya kumkinga dhidi ya maambukizi ya saratani ya mlango wa shingo la kizazi. (Kutoka kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw. Romuli Rojas John, Mkuu wa Idara ya Afya Dkt. Seleman Mtenjela).Bofya hapakupata kupata taarifa kamili:  http://www.mpandadc.go.tz/taarifa-kwa-umma