Friday, 1 June 2018

A default home page
MPANDADC.GO.TZ
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw. Hamadi Mapengo (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya madiwani na watalaam pamoja na wajumbe wa kamati ya afya Mwese wakiangalia eneo linalotarajiwa kujengwa majengo mapya ya kituo cha Afya cha Mwese. Serikali imetoa milioni 500 kwa kazi hiyo.


Viongozi Wakuu wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda wakiteta jambo kabla ya kuanza kikao cha baraza maalum. Baraza hilo limefanyika Mei 29, 2018 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri mhe. Hamadi Mapengo, Mkurugenzi Mtendaji Romuli John, Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mhe. Salehe Mhando, mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanganyika mhe. Yassin Kibiriti na makamu mwenyekiti mhe. Theodora Kisesa.


Wahudumu wa afya ya msingi wa kutoka Halmashauri ya wilaya ya Mpanda na Nsimbo wakipatiwa mafunzo katika ukumbi wa Lyamba.Mafunzo hayo yameendeshwa na waratibu wa huduma ya mama na mtoto kwa kufadhiliwa na taasisi ya Jane Goodall (JGI).Madiwani wakifurahia jambo la maendeleo katika kikao cha baraza maalum. Baraza hilo limefanyika Mei 29, 2018 na lilifadhiliwa na taasisi ya Jane Goodall (JGI)


Mkurugenzi wa taasisi ya Jane Goodall Bw. Emmanuel Mtiti akiwashukuru wajumbe wa CMT ya Halmashauri ya Mpanda (hawapo pichani). Watumishi wamejengewa uwezo wa kufanya kazi kwa kushirikiana kwa kila idara ili kuweza kutekeleza lengo la kupunguza ongezeko la watu na kufanikisha utunzaji wa mazingira.


Wajumbe wa CMT wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo ya kikao kazi cha namna ya kufanya kazi kwa kushirikiana kwa pamoja. Kikao hicho kimeendeshwa na taasisi ya Jane Goodall (JGI) katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda, Mei 30, 2018. Wa tatu kutoka kulia (mstari wa mbele) ni Bi. Phoebe Samwel kutoka JGI.


SASA HIVI MOTO UNAENDELEA KUWAKA KATIKA MLIMA WA LIYAMBAMFIPA ULIOKO ENEO LA KATA YA KAREMA UNAWAKA MOTO BAADA YA KUWASHWA NA WATU WASIOFAHAMIKA NA ENEO LILILOZUNGUKA MLIMA HUO KUNA MAKAZI YA WATU. BAADHI YA WANAKIJIJI WAMEFANIKISHA KUJIKINGA NA MOTO HUO KWAKUKAA PEMBEZONI MWA NYUMBA ZAO WAKIJARIBU KUUZIMA MOTO HUO KWA MATAWI MABICHI USIJE ZURU NYUMBA ZAO.
MWASLI LANGU JE MOTO HUU UNGEWAKA USIKU NANI ANGEJUA NA KUPAMBANA NAO?Wednesday, 23 May 2018

Halmashauri ya wilaya ya Mpanda imekabidhiwa magari 2 na kumpyuta 25 kutoka serikali Kuu. Vitendea kazi hivyo vimekabidhiwa na mbunge wa Mpanda vijijini mhe. Moshi Kakoso Mei 19, 2018 katika viwanja vya shule ya msingi Mpandandogo.
Gari moja aina ya ‘Toyota landcruiser-picup’ iliyotolewa na wizara ya maliasili na utalii kwa lengo la kulinda misitu na vyanzo vya maji katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda. Gari nyingine ni la kubebea wagonjwa lililotolewa na wizara ya afya, wazee, jinsia na watoto.
Hata hivyo katika hafla hiyo, Mkuu wa uendeshaji mfuko wa mawasiliano kwa wote(UCSAF) mhandisi Albert Richard amekabidi kompyuta 25 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda zenye thamani ya shilingi milioni 50. Baada ya kupokea kompyuta hizo zikakabidhiwa kwa wakuu wa shule za sekondari na moja kwenda kituo cha polisi Mishamo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Romuli Rojas John alishukuru kwa kupata magari hayo 2 na kompyuta 25. Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ina eneo kubwa kiutawala na maeneo mengi hayafikiki kiurahisi, kunahitajika magari mapya na yenye uwezo wa kuhimili changamoto za barabara zetu.
“Kwa mkoa wa Katavi, Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ndiyo halmashauri yenye eneo kubwa kuliko Halmashauri zingine. Nusu ya eneo la Halmashauri ni misitu tengefu na ushoroba. Nina watendaji vijana na wasomi wenyeuwezo wa kutunza vizuri vitendea kazi hivi.” Alisema Romuli
Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ina magari mengi makukuu na baadhi yameegeshwa kutokana na kuhitaji matengenezo makubwa na kwa gharama kubwa. Kwa mwaka wa fedha 2017/2018 tumepata magari mapya 3.


Mbunge wa Mpanda vijijini mhe. Moshi Kakoso(wa kwanza kutoka kulia) amepokea kompyuta 25 zenye thamani ya mil. 50 kutoka mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF). Akikabidhi kompyuta hizo, Mhandisi Albert Richard amesema kuwa kompyuta hizo zitasaidia kuinua taaluma ya wanafunzi wa shule za sekondari zilizopo katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda.


Mkurugenzi Mpanda DC akabidhiwa magari 2
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda, Romuli Rojas John ( wa kwanza kutoka kushoto) amekabidhiwa funguo za magari mawili kutoka kwa Mbunge wa Mpanda vijijini mhe. Moshi Kakoso. Magari hayo yametolewa na serikali kuu kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda.


Wajumbe wa kamati ya afya Mwese
Wajumbe wa kamati ya afya Mwese wamejipanga kukamilisha ujenzi na ukarabati wa kituo cha afya kwa wakati. Hayo yalisemwa mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wakati wa ziara ya kikazi iliyofanyika Mei 18, 2018.


Serikali yatoa Mil. 900 vituo vya afya Mwese, Mishamo

Serikali ya awamu ya 5 imeleta neema ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya vya Mishamo na Mwese. Kituo cha afya cha Mishamo kimepata milioni 400 za kujenga wodi ya kina mama, chumba cha kuhifadhia maiti, maabara, sehemu ya kuchomea taka ngumu na miundombinu mingine inayohusiana na afya.
Ujenzi wa kituo hicho unaenda vizuri na sasa umefikia katika hatua za umaliziaji. Wananchi wamejitoa sana katika kusomba mawe na matofali.
Wakati kituo cha afya cha Mwese kimepata shilingi milioni 500 na tayari zimeshaingia katika akaunti ya kijiji tangu Mei 9, 2018. Wananchi wa kata ya Mwese wameshaweka mikakati ya kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa nyumba 9 za wahudumu wa afya zinakamilika mapema.